Dada wa Bilionea Msuya Auawa Kinyama Dar
Posted by data tz
on Friday, May 27, 2016
0
Mtumishi wa Wizara ya Fedha, Aneth Msuya (30) ambaye ni mdogo wa Bilionea Erasto Msuya aliyeuawa kwa kupigwa risasi 22 KIA, ameuawa kwa kuchinjwa nyumbani kwake eneo la Kigamboni jijini Dar Es Salaam.
Mmoja wa ndugu wa
familia hiyo, Shujaa Khamis, jana alithibitisha kuuawa kwa Aneth,
lakini alikataa kuingia kwa undani.
“Ni
kweli wamemchinja usiku wa kuamkia leo (jana) na hapa nipo kwenye msiba
hapa nyumbani (Mererani) kwa baba. Tumeambiwa wamechukua Tv tu,” alisema.
Hata
hivyo, Khamis alikataa kueleza lolote kama wana mashaka na mauaji hayo
zaidi ya kuliomba Jeshi la Polisi nchini, kuchunguza kiini cha mauaji
hayo na kuwasaka waliohusika.
Habari nyingine kutoka Wizara ya
Fedha, ziliwakariri baadhi ya watumishi wakisema wamepata taarifa za
msiba huo, lakini hawajapewa taarifa rasmi.
“Tuna taarifa
tunazisikia sikia kuwa ameauawa, lakini jana (juzi) tulikuwa naye kazini
ila leo (jana) ndiyo tunasikia amechinjwa na watu wasiojulikana.
Imetusikitisha sana,” alisema mmoja wa watumishi hao ambaye hakutaja
jina kwa kuwa si msemaji.
Kamanda wa mkoa wa Kipolisi wa Temeke,
Andrew Satta alipofutwa jana kuthibitisha taarifa za mauaji hayo
alisema yuko kwenye kikao.
Tagged as:
Ni mtandao wa Kuhamasisha,Kuwawezesha Wajasirimali wadogo na wakubwa waweze kupata soko la Bidhaa/Huduma zao kwa Njia ya mtandao wa internet. Tunawatengezea vitabu, mashapisho na kurasa za Facebook, Instagram, Twitter. Wasiliana nasi kwa Email datatz88@gmail.com Simu 0763491136/0714067875/0688496762
Asante na Karibu Sana.
Jiunge Nasi
Jiunge nasi Upokee makala za kuhamasiha moja kwa moja kwenye email yako
Share This Post
Related posts
0 comments: