TAARIFA YA PILI YA WACHUMI NA WANASHERIA IMEBAINI KUWA KAMPUNI YA ACACIA MINING PLC HAINA KIBALI NA INAFANYA KAZI KINYUME CHA SHERIA
Posted by Unknown
on Monday, June 12, 2017
0

Prof. Osoro amesema kwamba Kamati yake imebaini kuwa Acacia haina uhalali wa kufanya shughuli zake hapa nchini na imetenda makosa yakiwemo kujipatia mali kwa udanganyifu, uhujumu uchumi, jinai na kuitia hasara taifa.
Aidha Kamati ya Prof. Osoro imebaini kwamba Makinikia yaliyouzwa nje ya nchi hayakuwa makinikia hasa, bali yalikuwa ni madini mbalimbali huku ikiongeza kwamba katika mikataba ya uuzwaji wa makinikia hayo, serikali haikuwa sehemu ya mikataba hiyo.
Prof. Osoro ameongeza kwamba jumla ya mapato yote ambayo serikali imepoteza ni Tsh. trilion 68.6 sawa na bajeti ya miaka miwili ya nchi kodi ya mapato ambayo taifa imepoteza ni Tsh. tril 55.07, mrahaba tril 11, bandari tril 1.6. na kwamba jumla ya thamani ya madini kwenye makontena yote 44,277 tangu mwaka 1998 ni Tsh. tril 132.56.
Pamoja na hayo imebainika kuwa uongezwaji wa leseni kinyume cha sheria ambapo imedaiwa kuwa aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja na Sospeter Muhongo ndio waliohusika na uongezaji wa muda kwenye uchimbaji wa madini.
Kamati hiyo imetoa mapendekezo mbalimbali ikiwepo kuchukua sheria juu ya kampuni ya ACACIA iliyopo nchini kinyume cha sheria kupitia msajili wa makampuni ikiwa ni pamoja na Mawaziri wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine juu ya mikataba ya uchimbaji madini huku ikiitaka Serikali iwe inafanya ukaguzi wa mara kwa mara kwenye makampuni ya madini
Tagged as: HABARI TANZANIA
Ni mtandao wa Kuhamasisha,Kuwawezesha Wajasirimali wadogo na wakubwa waweze kupata soko la Bidhaa/Huduma zao kwa Njia ya mtandao wa internet. Tunawatengezea vitabu, mashapisho na kurasa za Facebook, Instagram, Twitter. Wasiliana nasi kwa Email datatz88@gmail.com Simu 0763491136/0714067875/0688496762
Asante na Karibu Sana.
Jiunge Nasi
Jiunge nasi Upokee makala za kuhamasiha moja kwa moja kwenye email yako
Share This Post
Related posts
0 comments: