Waziri Mkuu Atoa ONYO Zito Kwa Wanaume Wanaowapa Mimba Wanafunzi

Posted by data tz on Tuesday, June 6, 2017 0

Tuesday, June 6, 2017

Waziri Mkuu Atoa ONYO Zito Kwa Wanaume Wanaowapa Mimba Wanafunzi



Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema mtu yeyote atakayebainika amemkatisha mwanafunzi wa kike masomo kwa kumpa mimba au kumfanyia vitendo vya ukatili vitakavyopelekea kukatisha masomo yake ni lazima afungwe miaka 30 jela.

Majaliwa ametoa agizo hilo leo Lugalo jeshini Jijini Dar es Salaam wakati akizindua na kukabidhi vifaa vya maabara na vifaa vya wanafunzi wenye mahitaji maalumu vyenye jumla ya thamani ya Shilingi Bilioni 16.9 kwa ajili ya shule 1696 kwa nchi nzima kwa lengo la kuhakikisha uboreshaji wa masomo ya sayansi.

Vilevile Majaliwa ameiagiza TAMISEMI kuhakikisha wanakamilisha maabara za shule zote nchini 4587 ambazo bado hazijakamilika ili vifaa hivyo vianze kusaidia wanafunzi kwa haraka na kufikia malengo ya nchi ya kuwa ya uchumi wa kati.

Pamoja na hayo, Majaliwa amesema watendaji watakaoenda kinyume na maadili ya kazi zao ni lazima mkono wa sheria uchukue nafasi yake.

Tagged as:
DataTz Group

Ni mtandao wa Kuhamasisha,Kuwawezesha Wajasirimali wadogo na wakubwa waweze kupata soko la Bidhaa/Huduma zao kwa Njia ya mtandao wa internet. Tunawatengezea vitabu, mashapisho na kurasa za Facebook, Instagram, Twitter. Wasiliana nasi kwa Email datatz88@gmail.com Simu 0763491136/0714067875/0688496762 Asante na Karibu Sana.

Jiunge Nasi

Jiunge nasi Upokee makala za kuhamasiha moja kwa moja kwenye email yako

Share This Post

Related posts

0 comments:

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();
© 2015-2016 DATA TZ GROUP. WP Theme-junkie converted by Bloggertheme9
Blogger templates. Proudly Powered by Blogger.
back to top