SIRI YAKUISHI MIAKA MING AU KUPATA UMRI MREFU
Posted by DataTZ
on Sunday, December 17, 2017
1
Kuishi karne moja au zaidi duniani ni mafanikio makubwa katika maisha ya binadamu lakini kutokana na kuongezeka sababu zinazopelekea mtu kufa mapema ikiwemo hali ngumu ya maisha na kukosa furaha na amani, imeelezwa kuwa ili uishi muda mrefu ni lazima ufanikiwe katika afya.
Sababu 7 ambazo zikizingatiwa zinaweza kumfanya mtu akaishi kwa
muda mrefu zaidi.
1:
Kutembea sana kwa miguu
George Boggess hakufikisha miaka 105 lakini aliishi zaidi ya
miaka 100 aliwahi kutoa ushauri na siri ya kuishi umri mrefu kuwa ni kutembea.
2:
Kula samaki na kulala kwa angalau saa 8
Misao Okawa, ambaye alitambulika kama binadamu mkwenye umri
mkubwa zaidi dunia ambaye alifariki akiwa na umri wa miaka 117 alisema sushi
(samaki) na saa 8 za kulala ni siri ya kuishi kwa muda mrefu. Wajapan wanatajwa
kuwa na uwiano wa kuishi muda mrefu mbapo kuna zaidi ya watu 5,000 wanaosemwa
kuishi zaidi ya mika 100.
3: Kupiga push-ups tano hadi saba kila siku
Duranord Veillalord ambaye alitimiza miaka 109 mwaka jana
anaianza siku yake kwa pushups kila siku. Pushups, kikombe cha chai na matunda
ni siri ya kuishi kwa miaka mingi.
4:
Kaa mbali na vipodozi
Adelina Domingues alikuwa mtu mwenye umri mkubwa zaidi kuwahi
kuishi Marekani ambapo alifariki akiwa na umri wa miaka 114 anasema siri kubwa
ya yeye kuishi miaka mingi ni kujiweka mbali na vipodozi.
5:
Kunywa uji wakati wa kufungua kinywa
Jesse Gallan aliishi kwa miaka 109 na kusema siri kubwa ilikuwa
kunywa uji kama kifungua kinywa chake pia alisema kutokuwa na wanaume wengi
kwenye maisha yake kuliongeza miaka ya maisha yake.
6:
Kaa mbali na pombe/ulevi
Alexander Imich wa New York City ambaye aliishi kwa miaka 111
alisema siri kubwa ya yeye kuishi miaka 111 ni kwa sababu alijiweka mbali na
kilevi na alikuwa muogeleaji na kufanya mazoezi. Chakula chake kilikuwa ni kuku
na samaki na kuishi maisha ya kuzingatia kanuni za kiafya.
7:
Kula kwa kiasi
Wanawake wa jamii ya Hunza inayopatikana katika mipaka ya
Kashmir, China na Afghanistan hupata watoto wakiwa na miaka 60 na wanaume
wanaoonekana kama wana miaka 40. Wazee wa jamii hii wamefikisha umri wa miaka
mia moja na wangali na muonekano kana kwamba wana miaka 70 ambapo wanajamii
hiyo wakisema siri ni kula kwa kiasi. Wanakula nyama kidogo katika milo miwili
kwa siku.
Tagged as: HABARI TANZANIA
Ni mtandao wa Kuhamasisha,Kuwawezesha Wajasirimali wadogo na wakubwa waweze kupata soko la Bidhaa/Huduma zao kwa Njia ya mtandao wa internet. Tunawatengezea vitabu, mashapisho na kurasa za Facebook, Instagram, Twitter. Wasiliana nasi kwa Email datatz88@gmail.com Simu 0763491136/0714067875/0688496762
Asante na Karibu Sana.
Jiunge Nasi
Jiunge nasi Upokee makala za kuhamasiha moja kwa moja kwenye email yako
Share This Post
Hello , for more info on how to stay ahead of others visit above20ceo.blogspot.com
ReplyDelete