Miliki Website / Blog / PhoneApp
Website/Blog ni nini?
Website/Blog ni mtandao/tovuti/ukurasa ambao unatumia kuweka
habari endelevu za mara kwa mara. Mtandao huu unalenga Zaidi kumilikiwa na mtu
mmoja au kikundi kidogo cha watu.
Blog ni rahisi kutumia kuliko tovuti nyingine za
kawaida huhitaji mtu wa IT kwa ajili ya kukuendeshea unaweza kutumia mwenyewe
na kuendesha mwenyewe.
Blog haina gharama kubwa za kuendesha kama wewe ndio
unaanza unashauriwa kumiliki blog aina ya kawaida kabisa ambayo hulipii
chochote Zaidi ya gharama za kutengenezewa nayo itakua kama hivi www.datatz1.blogspot.com hiyo ni blog ambayo
utatumia bure hadi utakapoamua kubadilisha na kulipia domain ambapo itakua hivi www.datatz1.com ni wewe mwenyewe kuchagua aina
unayotaka ila kwa wale ambao bado kabisa ndio wanaanza kutumia mtandao huu
nawashauri kuchukua ambayo haina malipo ya mwezi ili kupata uzoefu kwanza.
Blog ni nzuri kwa kutunza kumbukumbu zako haijalishi
unaandika kitu gani kwa kupitia blog utaweza kutunza kumbukumbu zako muda mrefu
sana bila kupoteza na ni sehemu ambayo hakuna wa kukuingilia wewe ndio mmiliki.
Ni sawa na ofisi yako ni sehemu ambayo wewe unaamua uweke nini na ukitunze vipi.
Mtu gani anatakiwa amiliki blog? Naweza kusema
ni kila mtu ambaye anafanya vitu vinavyomkutanisha na watu. Haijalishi ni
biashara, kazi yako, kipaji chako, au chochote kile kumiliki blog ni muhimu
kwasababu uliwengu wa sasa unahamia kwenye mtandao kama huna mtandao utaachwa
nyuma sana.
Blog haihitaji uwe na uelewa mkubwa sana wa IT. Watu
wengi wanaogopa kwamba hawataweza kuendesha blog kwakua hawajui kutumia
computer ukweli ni kwamba mambo ni marahisi sana unaweza kuendesha blog kwa
kutumia smartphone yako, tablet na computer ni ufahamu kidogo sana unahitajika
juu ya uendeshaji.
Mitandao ya kijamii.
Kitu cha pili ambacho ni muhimu kua nacho ni
kurasa kwenye mitandao ya kijamii kurasa hizi zinakuwezesha wewe kuwaelekeza watembeleaji
wako kwenye blog yako. Kuna aina mbalimbali ya mitandao ya kijamii kama
Facebook. Twitter Instagram, Whatsapp na Telegram. Watu wengi wamekua na
matumizi mabaya na hii mitandao. Naomba wewe usiwe mmoja wao itumie mitandao
hii kwa namna bora ya kusaidia watu na wewe mwenyewe uweze kupata manufaa.
Tumia vyema wale watu unaokutana nao ili uweze kunufaika na wao wanufaike pia.
Kama ni biashara utahitaji uwe na ukurasa
kwenye Facebook ukurasa ambao utasimama kwa jina la biashara yako. Utajieleza
ni kitu gani unafanya na watu wakaotembelea ukurasa huo watapata mawasiliano
yako na kukutafuta.
Pili utahitaji uwe na ukurasa kwenye Instagram
wenye jina la biashara yako. Hapa utakua unaweka picha za bidhaa au huduma
uanzotoa au wewe mwenyewe. Hii inawavuta watembeleaji waone kitu halisi
unachokifanya.
Kwa wale ambao wanatumia groups za whatsapp
kuweka maelezo ya bidhaa zao au kuweka mafundisho si vibaya ila inaweza kua ni
upotevu wa kazi zako kama hujazitunza sehemu nyingine. Ukimiliki blog mtu
yeyote anaweza kutembelea hata kama hayuko kwenye mtandao wowote pale tu
unapompatia link ya ukurasa wako.
Katika kipindi hiki cha karibuni kumekua
na watumiaji wengi sana wa mtandao wa internet hasa baada ya kuja kwa wingi kwa
simu za mkononi aina ya smartphone kwa maisha ya sasa karibia kila mahali
unapokwenda huwezi kumkosa mtu na simu yenye uwezo wa internet.
Usiogope kuchukua hatua hata kama hujui
chochote tutakufundisha ili uweze kufaidika na mabadiliko haya. Huko tuendako
tutafika mahali lazima ujue kutumia mtandao maana huduma nyingi zitakua
zinatolewa kwa njia ya mtandao. Sasa hivi tuaendesha semina kwa njia za
mtandao. Kwenye groups za Whatsapp na Telegram. Dunia inafika sehemu ambapo
lazima kila mmoja abadilike kuyafuata mabadiliko la sivyo utaachwa nyuma sana.
Faida za kumiliki blog:
Biashara/Kipaji chako kutambulika kimataifa
Blog inawezesha biashara/huduma au kipaji chako
kutambulika kimataifa kwa kua mtu yeyote popote duniani anaweza kutembelea blog
yako na akaona kazi/huduma zako au bidhaa unazotoa au kile unachokiandika, hii
itaifanya biashara yako kipaji chako au maandishi yako yatambulike zaidi na
watu wengi hata usiowajua.
Utunzaji wa kumbukumbu
Chochote utakachokiweka kwenye blog yako
kitakua salama hivyo basi kumbukumbu zako zinakua salama. Unaweza kuandika
kwenye blog na kujitengenezea watembeleaji na kufungua fursa mbalimbali hapa
Tanzania na nje ya nchi. Kumbukumbu zako utakua nazo wewe na utaweza kuacha
alama duniani hata siku ukiondoka.
Kuacha alama.
Unapomiliki blog unaacha alama duniani blog
yako itaendelea kua hai na yale uliyoayaandika yatakuwepo. Nimeona shuhuda
mbalimbali za watu waliosoma Makala kwenye mitandao wakachukua hatua zikabadili
maisha yao, hivyo hata wewe unaweza kuacha alama, sio biashara pekee yake
unaweza kumiliki blog kwa ajili ya kitu chochote unachotaka jamii ifahamu ni
wewe unakifanya.
Inakujengea nidhamu
Unapokua na blog yako unaandika kuhusu kitu
Fulani ni muhimu ujiwekee ratiba maaalumu ya kuandika kama ni kila siku au kwa
wiki mara moja vyovyote vile itakujengea wewe nidhamu binafsi ya kufanya
mambo mengine pia. Unaweza
kuanzisha pia groups za Whatsapp ambazo ni kwa ajili ya watu wanaosoma vitu
unavyoviandika.
KUTENGENEZA PESA
Ukimiliki blog unaweza kutengeneza pesa sana
kama tulivyoona faida nyingine, unatengeneza pesa kwa huduma utakazo kua
unazitoa, unaweza kutengeneza vitabu vilivyopo kwenye mfumo wa pdf ambapo
wasomaji wako utawauziwa kwa njia ya email, unaweza kuendesha semina za online
wasomaji wako wakalipia, unaweza kuuza bidhaa zako sehemu mbalimbali kwa
watembeleaji wako, cha muhimu ni uvumilivu kwa kua haya hayatokei ndani ya siku
moja bali yanaletwa na uaminifu uliojengeka kati yako wewe na watembeleaji wako.
Data Tz Group inakuwezesha wewe na watu wako unaotaka waone
kile unachokifanya kwa kukupa huduma nzuri ya kutengenezewa blog na
utakayoweza kuendesha mwenyewe. Unachotakiwa kufahamu ni kutumia simu yako ya
kiganjani (smartphone) au computer yako.
www.datatz1.blogspot.com
Gharama yake ni Tsh 50,000 ambapo hutalipia tena baada ya hapo kama unataka
ibaki hivyo hivyo.
www.datatz1.com Gharama yake ni tsh 100,000/= na utakua unalipia Tsh 30,000/= kila mwaka baada ya mwaka wa kwanza. Tofauti yake ni kwamba unakua umenunua Domain ya jina unalolitaka na ile blogspot inaondoka, hivyo unachokilipia kila mwaka ni hilo jina.
Vitu Utakavyopata tofauti na Blog ni
(a) Ukurasa wa Facebook wa Biashara yako au Jina
lako.
(b)
Mail List hii ni sehemu watu unaofanya nao
biashara wanapojiunga hivyo unakuwa na uwezo wa kuwasiliana nao.
(c) Mbinu mbalimbali za kukusanya watembeleaji
kwenye blog yako.
(d)
Muonekano Bora wa Blog Yako pamoja na maelekezo
juu ya kutumia.
(e)
Utapata Email kama umenunua domain name na itakua ni fowarding email
au yenye mailbox ya kujitegemea chaguo ni lako.
Mawasiliano yetu
Simu: 0763491136 (WhatsApp)
Email: boniface.yohana@yahoo.com
Unatengenezewa blog popote ulipo duniani
unatuma pesa kwa njia ya simu M Pesa O763491136 Tigo pesa
0714067875 majina ni Boniface Yohana kisha unatuma ujumbe mfupi wenye majina yako
pamoja na maelezo kuwa umenitumia pesa.
Kwa walio nje ya nchi unaweza kuwasiliana nami
kwa njia ya email boniface.yohana@yahoo.com au kwa
Whatsapp +255 763491136
Asante sana na Karibu.
HIZI HAPA NI BAATHI YA BLOG NILIZOWATENGENEZEA WATU BINFSI NA VIKUNDI MBALI MBALI.
1. Data Tz GROUP
2. KILIMO TIJA
3. ECONOMIC NEWS
4. TORL GARDEN PLANNERS
5 CCM BOKORANI
6. PAVEA BLOG
Nimekupata mkuu
ReplyDeleteyap yap
Deletepoa poa mkuu tupo pamoja
ReplyDelete