TOFAUTI YA UWEKEZAJI WA HATIFUNGANI (BOND) NA MASOKO MENGINE YA MITAJI KAMA HISA(SHARE).

Posted by data tz on Thursday, June 9, 2016 0

Hatifungani ni tofauti kabisa na masoko mengine ya mitaji kwa mfumo wake na hata faida zake.

💥Kwenye hatifungani unapata faida bila ya kujali uchumi unakwendaje. Kwa sababu unaponunua hati fungani unajua kabisa ni riba kiasi gani unapata kwa mwaka. Lakini kwenye hisa hujui ni faida kiasi gani unapata kwenye uwekezaji wako. Faida inategemea na halinya uchumi, uimara wa soko.

💥 Kwenye hisa unapata faida pale hisa zinapofanya vizuri na unapata hasara pale hisa zinapofanya vizuri. Kwenye hatifungani unapewa riba uliyoambiwa bila ya kujali fedha ulizowekeza zimezalisha au la.

💥 Kwenye hisa unaweza kupata faida kubwa sana pale uchumi unapokwenda vizuri. Kwenye hatifungani utapata riba ile ile.

💥 Hatifungani zina kipindi maalumu baada ya hapo zinakomaa na hivyo kurudishiwa fedha zako. Hisa hazina ukomo wa kipindi, kadiri kampuni inavyoendelea kuwepo unaweza kuendelea kumiliki hisa zake.

💥 Kwenye hisa unaweza kushiriki kwenye vikao mbalimbali vya kampuni, kwenye hatifungani hupati nafasi hiyo. Wewe unawekeza fedha na kuchukua riba mpaka pale inapokomaa.

#Hii ni sehemu ya mafunzo ya DARASA LA LEO IJUMAA kwenye Data Tz kuhusu uwekezaji kwenye HATIFUNGANI (BONDS).
Image result for bond and share image

Tagged as:
DataTz Group

Ni mtandao wa Kuhamasisha,Kuwawezesha Wajasirimali wadogo na wakubwa waweze kupata soko la Bidhaa/Huduma zao kwa Njia ya mtandao wa internet. Tunawatengezea vitabu, mashapisho na kurasa za Facebook, Instagram, Twitter. Wasiliana nasi kwa Email datatz88@gmail.com Simu 0763491136/0714067875/0688496762 Asante na Karibu Sana.

Jiunge Nasi

Jiunge nasi Upokee makala za kuhamasiha moja kwa moja kwenye email yako

Share This Post

Related posts

0 comments:

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();
© 2015-2016 DATA TZ GROUP. WP Theme-junkie converted by Bloggertheme9
Blogger templates. Proudly Powered by Blogger.
back to top