Posted by data tz
on Wednesday, June 7, 2017
0
Wednesday, June 7, 2017
Mwanasheria Mkuu wa TBS Afikishwa Mahakamani
Mwanasheria Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Baptister Marco (54) amepandishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashtaka matatu ya kuishi na kufanya kazi nchini bila kuwa na kibali.
Mwendesha Mashtaka wa Uhamiaji, Novatus Mlay alimemsomea mashtaka hayo leo Jumatano kwa Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa.
Akisoma hati ya mashtaka, Mlay alidai kuwa Mei 19, 2017 huko Kinondoni katika ofisi ya uhamiaji, Marco akiwa raia wa Burundi alikutwa nchini bila kuwa na kibali cha kumuwezesha kuishi.
Marco katika shtaka la pili amedaiwa kuwa siku hiyo alikutwa akifanya kazi kama Mwanasheria Mkuu wa TBS bila ya kuwa na kibali kinachomruhusu kufanya kazi hapa nchini.
Katika shtaka la tatu, Mlay alidai kuwa, Julai 6 mwaka 2011 katika ofisi ya Uhamiaji ya Dar es Salaam iliyopo Wilaya ya Ilala, mshtakiwa huyo akiwa raia wa Burundi alitoa taarifa za uongo kuhusu maelezo yake binafsi wakati akijaza fomu ya kuomba hati ya kusafiria namba CT (5)(Ai).
Wakili Mlay alisema kitendo hicho cha kutoa taarifa za uongo kilimuwezesha Marco kupata hati ya kusafiria ya Tanzania yenye namba AB 474856 huku akijua kufanya hivyo ni kinyume cha sheria za nchi.
Baada ya kusomewa mashtaka hayo, alikana na upande wa mashtaka ulidai kuwa upelelezi bado haujakamilika.
Mshtakiwa alitakiwa kuwa na wadhamini wawili wanaoaminika ambao kila mmoja atasaini bondi ya Sh 20 milioni na alikamilisha. Kesi imeahirishwa hadi Juni 21, 2017 kwa ajili ya kutajwa.
Tagged as: HABARI TANZANIA
Ni mtandao wa Kuhamasisha,Kuwawezesha Wajasirimali wadogo na wakubwa waweze kupata soko la Bidhaa/Huduma zao kwa Njia ya mtandao wa internet. Tunawatengezea vitabu, mashapisho na kurasa za Facebook, Instagram, Twitter. Wasiliana nasi kwa Email datatz88@gmail.com Simu 0763491136/0714067875/0688496762
Asante na Karibu Sana.
Jiunge Nasi
Jiunge nasi Upokee makala za kuhamasiha moja kwa moja kwenye email yako
Share This Post
Related posts
0 comments: